SIRI ZA BIBLIA: NGUVU ZA MADHABAHU/MAAGANO NA MIKATABA YA KUZIMU
Manage episode 313499879 series 3273506
Kumekuwa na mitazamo mingi ya tofauti tofauti ya namna ya kushughulikia matatizo sugu ambayo yamewakabili watoto wa Mungu kwa muda mrefu sana. Kuna watu wametaka kutoka katika umasikini kwa muda mrefu lakini hawajatoka mpaka sasa na hawajui tatizo limekaa wapi, wengine wametaka kutoka katika matatizo ya ndoa, wengine wametaka kuoa au kuolewa lakini mambo hayo yameshindikana kabisa hata kwa kufunga na kuomba hawajaweza kutoka katika matatizo hayo na mpaka sasa hawana majibu ya matatizo yao. Kuna watu familia zao zimekuwa na vifo vya kutatanisha au vya ghafla, wengine wamekuwa na magonjwa ya kutisha kutoka kizazi hadi kizazi na hata sasa hawana majibu ya maswali yao.
Matatizo sugu huwa chanzo chake na hayatokei pasipo chanzo/sababu. Chanzo au msingi wa matatizo sugu ni kuvunjika kwa makubaliano (maagano/mikataba) yaliyoingiwa na pande mbili au zaidi, anayevunja makubaliano anaingia kwenye matatizo ambayo ni matokeo yaliyokubaliwa (kwa kujua au bila kujua) wakati wa kufunga mkataba/mikataba hiyo (Kumbukumbu 28:15-68 “15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata…………..”). Kwa utaratibu na sheria za kiroho mikataba/maagano hayo hufanyika katika madhabahu ambazo ndio kiunganishi kati ya ulimwengu wa mwili na ulimwengu madhabahu hizi huonekana kwa macho ya kibinadamu (kwakuwa hujengwa katika ardhi)
--- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message119 ตอน