SIRI ZA BIBLIA: MFAHAMU LILITH,MALKIA WA KUZIMU ALIYEASI BUSTANINI
Manage episode 313499889 series 3273506
Lilith ni jina la mwanamke ambaye katika hadithi fulani za Mesopotamia ya kale anatajwa kama mungu mke ambaye anahusika na dhoruba akazaa majini.
Biblia inasimulia jinsi dunia ilivyoumbwa na mwanzo wa binadamu. Katika maandiko hayo, masimulizi ya uumbaji yana changamoto kuyafahamu sawasawa, hususani kitabu cha Mwanzo 1:26 na Mwanzo 2. Uumbaji wa mwanamke unatajwa sehemu hizo mbili, lakini kwa namna tofauti, kwa kuwa ni visasili tofauti. Katika Mwa 1:26 Mungu aliwaumba Adamu na Eva sawia kwa sura na mfano wake. Katika Mwa 2 Mungu anamuumba Hawa baada ya kuchukua ubavu wa Adamu na kumfanya mwanamke.
Katika Biblia Isa 34:14 tu inamtaja Lilith, na jina hilo linatafsiriwa pengine "Bundi", sambamba na wanyama wengine saba wanaotajwa katika mstari huohuo na ule unaofuata.
Hata hivyo kuanzia karne ya 10 BK wametokea watu wanaodai Lilith, si Hawa, ndiye mwanamke wa kwanza ulimwenguni naye aliumbwa na Mungu wakati mmoja na Adamu. Wanasema Lilith alifukuzwa na kukataliwa na Mungu baada ya kupatikana kuwa mwenye nguvu zaidi na mwenye akili zaidi ya Adamu na hakutii amri za Adamu.
--- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message119 ตอน